![]() |
Unakumbuka ile kolabo ya P Square na Akon inaitwa Chop my money ambayo ilimfanya May D kuwa staa zaidi baada ya kuongezwa kuwa mtu wa nne kusikika kwenye hiyo single? kama hufahamu May D ni msanii wa Nigeria ambae alisainiwa kuwa chini ya lebo inayomilikiwa na P Square (Square Records) ambapo ni siku kadhaa zimepita toka lebo hiyo itangaze kwamba haimuhitaji tena na wala hayuko tena chini yao. Leo mtandao wa Naijag umeripoti kwamba May D ambae alitimuliwa na lebo hiyo wiki kadhaa zilizopita yuko kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na wanasheria wake ili awashitaki P Square kwa kuvunja mkataba kiholela. May D anasema taarifa za kutimuliwa kwake alizipata kwenye blogs na magazeti kama walivyopata watu wengine na kwamba hakupewa taarifa zozote za kiofisi kama inavyopaswa, hiyo ndio sababu inayomfanya awashitaki P Square akiwemo kaka yao mkubwa Jude Okoye ambae ndio alitangaza kuuvunja mkataba wa May D. Source; millard ayo |
Sunday, September 9, 2012
TAARIFA KAMILI KUHUSU PSQUARE KUSHTAKIWA...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment