Ads 468x60px

.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

FOLLOW US ON TWITTER

FOLLOW US ON TWITTER

.

Monday, August 27, 2012

AMAZING SNAKE WOMAN

THT - SERENGETI FIESTA 2012

KAMA UMEKOSA EBSS EPISODE 2 - LINDI - ARUSHA AUDITIONS HII INAKUHUSU!!!

LIVERPOLL V.S MANCHESTER CITY 2-2

FIESTA TANGA HAPATOSHI USIKU HUU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

SCORPION GIRLS!!!!

Al-Shabaab Yaamua Kuuza Nyama Ya Fisi ili Kugharimia Operesheni Zao Za Kijeshi

Wafanya biashara wa al-Shabaab wanawaambia wakazi wa Kismayu kuwa kula nyama ya fisi itawalinda na maradhi na jicho la uovu. Juu, mwanamke anauza nyama huko Dinsor.
Al-Shabaab wameanza kuuza nyama ya fisi katika mji wa bandari kusini ya Somalia kama njia ya kukusanya pesa kwa ajili ya operesheni za kijeshi kabla ya kukaribia kwa vita dhidi majeshi ya Somalia na washirika wake , wachambuzi wasema.
Masheikh wa Somalia ambao kwa karne nyingi wamekuwa wakichukulia kuwa ulaji wa nyama ya fisi kulikatazwa na Uislamu kwa vile mnyama huyu hula miili ya maiti wa kibinadamu na wanyama.
Hatua hii mpya ni moja ya dalili nyingi za kuchanganyikiwa kifedha kwa washirika wa kikundi cha al-Qaida wakati majeshi ya Somalia na washirika wake yanaendelea kuziteka kambi za al-Shabaab nchini kote.
Ili kuwashawishi wakaazi kula nyama hiyo, ambayo mara nyingi ina magonywa kwa sababu mnyama huyo anakula mizoga, wafanya biashara wa al-Shabaab wamekuwa wakitumia uchawi wa asili ili kuwanasa wale wasiofahamu vyema, alisema Suleiman Abdi Guled, mpishi katika Hotel Alkhalej mjini Mogadishu ambaye ana familia huko Kismayo.
Kwa mujibu wa watu wanaofanya uchawi, nyama ya fisi ni nzuri kwa kujikinga na maapizo na dhidi ya magonjwa na jicho la ubaya.
"Ni ishara ya kutisha kwa sababu ni nje ya mila [za Kisomali] kula nyama ya fisi, hasa kwa vile wapo wanyama wengine wa kuliwa," alisema. "Al-Shabaab ni kikundi kilichopotea ambacho kinajaribu kutumia fisi na uchawi kwa operesheni zao za kijeshi."
Khalif Mohamud, mfanya biashara wa Kismayo, alisema al-Shabaab wanapata pesa katika biashara hii kwa kuudhibiti uchinjaji wa fisi.
"Al-Shabaab wanayo majumba ya machinjio mjini na tunalazimika kulipa pesa kwa kuchinja na kuchuna wanyama baada ya mawindo," aliiambia Sabahi.
Nyama ya fisi -- imeruhusiwa au kukatazwa kidini ?
Sheikh wa Somalia Sheikh Mohamud Awabdulle Ariif alisema watu wamekatazwa kuwinda na kula nyama ya fisi kwa mujibu wa sharia.
"Fisi ni miongoni mwa wanyama wadanganyifu na walafi, kwa vile wanawinda kondoo na kula nyama ya binadamu," alisema. "Pia hufukua makaburi na kutoa na kula maiti, pamoja na kula mizoga ya wanyama, wadudu na mabaki ya mawindo mengine."
Mursal Issac, mwanaharakati wa jumuiya ya kiraia mjini Mogadishu, alisema hali mbaya ya kifedha ya al-Shabaab imekipelekea kikundi kuamua kufanya biashara ya mkaa na nyama ya fisi ili kugharimia operesheni zake za kijeshi.
"Fisi ni wanyama wachafu wanaokula mizoga ya wafu, na ndio sababu ninawataka ndugu zetu wa Kismayo kujizuia na kula nyama yao," aliiambia Sabahi. "Tumebarikiwa na Mungu ardhi na wanyama wa baharini, na nadhani ni bora kujiweka mbali na mnyama huyu."
Issac alisema al-Shabaab inajaribu kunyanyua hali yake mbaya ya kifedha kwa sababu inaogopa kushindwa kijeshi mikononi mwa Jeshi la Somalia na Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).
Sagal Hassan Ali, ambaye anafanya kazi katika mkahawa mdogo katika kiunga cha Via Afmadow, Kismayo, alisema yeye hatakula nyama ya fisi na hata asingewinda mnyama huyu muovu.
Aliiambia sabahi kuwa anachukizwa kuwa soko la hapo limegeuzwa uwanja wa kufanyia biashara ya nyama hii.

FIESTA TANGA KABLA YA SHOW!!!!!!!!!!!!





WORLD UGLIEST DOG...


Saturday, August 25, 2012

MATONYA AFARIKI DUNIA!!!!


Matonya akiwa na mwanae  Elilzabeth


 
LICHA ya umaarufu mkubwa aliokuwa nao na kufahamika katika miji mingi nchini, ombaomba Paul Mawezi maarufu kwa jina la Mzee Matonya, amefariki dunia na kuzikwa katika mazingira ya ufukara mkubwa.
Matonya alizikwa jana kijijini kwake Mpamantwa, Wilaya ya Bahi, Dodoma akiwa amevishwa nguo moja nyeusi, huku mwili wake ukibebwa na watu wasiozidi 20, waliotumia ngozi kuu kuu ya ng’ombe.
Matonya aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kikohozi tangu Mei mwaka huu, alifariki dunia juzi usiku na kuzikwa jana saa saba mchana mita tatu kutoka katika nyumba yake ya tembe alimokuwa akiishi.
Ndugu na jamaa zake wa karibu walisema Matonya ambaye umri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya miaka 90, hakuwahi kwenda kutibiwa hospitali kutokana na ukosefu wa fedha.
Mwandishi wetu alishuhudia idadi ndogo ya waombolezaji nyumbani kwa Matonya, huku watoto wake watatu waliokuwapo msibani hapo kati ya watano aliowaacha hai, wakisema kuwa baba yao amefariki kutokana na umaskini na ufukara.
“Hatukuweza kumpeleka hata hospitali kupata vipimo kwani hatukuwa na uwezo wa kwenda mjini Dodoma kutokana na kukosa hata nauli, ndiyo maana tumekuwa kimya hadi Mungu alipomchukua,’’ alisema mmoja wa watoto hao, David Paulo.
Umaarufu wa Matonya
Umaarufu wa Matonya ulitokana na staili yake ya kuomba kwa kulala chali barabarani, huku akiwa ameinua kopo juu bila ya kujali jua au mvua.
 Kwa nyakati tofauti alipinga mpango wa Serikali wa kumrejesha kwao Bahi na mara kadhaa alimweleza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusufu Makamba kuwa yeye ni mtoto wa mjini hivyo asingemuweza. Aliingia Dar es Salaam kwa mara ya kwanza Desemba 7, 1961.
Katika siku za karibuni, alikuwa gumzo kwa Serikali na viongozi huku akipachikwa jina la Komandoo na Kiboko ya Makamba.
Baada ya kuondolewa Dar es Salaam, aliweka makazi yake mapya ya kuomba mkoani Morogoro hususan eneo la Darajani, ambako aliendeleza staili ya kuomba akiwa amelala chali na kuinua kopo juu kwa muda mrefu bila kuchoka.
Iliwahi kuvuma kwamba ombaomba huyo alikuwa na utajiri mkubwa, jambo ambalo mtoto wake mkubwa, Elizabeth Paulo alilipinga na kusema kwamba halina ukweli na hakuacha chochote.
Mke wa Marehemu Paulina alisema walitengana na Matonya zaidi ya miaka 37 iliyopita na wakati huo alikuwa na mali nyingi (ng’ombe).
“Tulipotengana tu, mimi nilirudi kwetu na watoto wangu walikuwa bado wadogo na bahati mbaya mdogo wake aliyekuwa akitunza ng’ombe (wa Matonya) alifariki dunia na huo ukawa ndiyo mwanzo wa kumaliza mifugo yote kwani watu waliwaiba wote,’’ alisema Paulina.
Matonya alirudi kijijini kwake Mpamantwa kwa ajili ya mapumziko ya Krismasi Novemba, 2010 akitokea Morogoro kama ilivyokuwa kawaida yake na tangu wakati huo hakurudi tena.

Makamba, Mashishanga wamlilia
Akizungumzia msiba huo, Makamba ambaye alifanikisha mpango wa kumwondoa Matonya Dar es Salaam, alisema amesikitishwa na kifo hicho cha mtu aliyemtaja kuwa alikuwa rafiki yake mkubwa.
“Nasikitika nimempoteza rafiki mkubwa… Mimi nilimpenda lakini inaonekana Mungu amempenda zaidi,” alisema Makamba jana kwa simu.
Alisema urafiki wao ulianzia pale alipomwondoa Dar es Salaam na kumrejesha nyumbani kwao Dodoma, lakini baadaye akahamia Morogoro... “Alipokwenda Morogoro (Matonya) alisema ‘naipenda CCM, lakini simpendi Makamba.’ Waandishi waliponifuata wakaniuliza nikasema mimi nampenda,” alisema Makamba.
Alisema kauli yake ya kumpenda inathibitishwa na mkakati wake wa kutaka kumwondoa katika mazingira ya dhiki na jua kali wakati wa kuombaomba katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kumpeleka kwao Dodoma, ambako angeweza kutulia na kuishi vizuri na ndugu zake.
“Alikwenda huko, lakini kwa bahati mbaya kama Waswahili wasemavyo, mazoea yana tabu, akarejea kwenye kazi yake mkoani Morogoro,” alisema Makamba.
Makamba ambaye baadaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kabla ya kustaafu, alisema Matonya alikuwa mmoja wa makada wanaokipenda chama hicho tawala, hivyo licha ya kusikitika kupotelewa na rafiki, pia anasikitishwa na chama kumpoteza mmoja wa wakereketwa wake.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mstaafu, Stephen Mashishanga alisema, Matonya alikuwa mzee maarufu na hakuwa mtu aliyependa makuu kwani kila alipotakiwa kuondoka mjini alitii.
Alisema kifo chake kimemsikitisha kama binadamu mwenzake hasa akikumbuka kuwa hakuwahi kumnyanyasa, akisema alikuwa ombaomba aliyependa kukaa eneo moja na kila aliyemwonea huruma alitoa sadaka yake.
“Alipotakiwa kuondoka, aliondoka lakini baadaye alirudi mahali ambako kuna masilahi; Hata ng’ombe hukimbilia mahali ambako anajua kuna nyasi za kutosha,” alisema Mashishanga.
habari hii imetoka http:mwananchi.co.tz

INSPECTOR HAROUN - MBOGA SABA

BEN POL - PETE

CYRILL FT CHEGE - SIKUHIZI HATULALI

PAH ONE - ASAMBEENI

Monday, August 20, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA SWALA YA EID LEO!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa  wakati alipowasili katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam kwa ajili ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini mskitini. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda wakati alipowasili katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam kwa ajili ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012