Ads 468x60px

.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

FOLLOW US ON TWITTER

FOLLOW US ON TWITTER

.

Tuesday, November 27, 2012

I WISH R.I.P MEANS.. RETURN IF POSSIBLE, REST IN PEACE SHARO MILIONEA

GARI ALIPATA NAYO AJALI

GARI AINA YA HARRIER IKIONYESHA ILIVYO HARIBIKA BAADA YA AJALI..

SMS YA MWISHO NA LINEX KABLA YA MAUTI KUMFIKIA

SHARO MILLIONEA
Msanii maarufu kunako tasnia ya filamu za maigizo kwa upande wa vichekesho almaarufu kama Sharomillionea ameripotiwa kupata ajali maeneo ya Maguzini songa karibu na wilaya ya Muheza mkoani Tanga majira ya saa mbili usiku wa 26/11/212 na gari aina ya Toyota Harrier yenye namba za usajili T 478 BVR  ambalo kutokana na mwendokasi gari hiyo iliacha njia na kuvamia mti kwenye vichaka vya pembezoni mwa barabara na gari kupinduka na kufariki papo hapo na mwili wake kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Kutokana na chanzo chetu cha habari msanii huyo alikwenda Tanga kwa dhumuni la kumsalimia mama yake mzazi na kwa mapenzi ya Mungu hata kabla ya kuonana na mzazi wake mauti yalimfikia njiani humo.
Katika eneo la tukio kuna vitendo vya kusikitisha vilitokea ambapo wakati wa zoezi la kumnasua, vibaka waliweza kumpora simu alizokuwa nazo, fedha zenye thamani ya shilingi za kitanzania millioni sita na kumvua viatu na nguo alizovaa na kumuacha na nguo za ndani (boxer na vest) vile vile walimchukulia na saa yake ya mkononi. Wakazi wa kijiji hicho wamesikitishwa na kulaani vikali kitendo hicho. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwao muheza , Tanga. Nuru ya msanii huyu imezimika ghafla kwa maana alikua ameshaanza kushika kasi katika matangazo mbalimbali katika TV na redio stesheni mbalimbali pia kazi za comedians zikiwa zinakubalika sana na pia katika tasnia ya muziki wa Bongo flavour.
blog hii inatuma salamu za rambirambi kwa familia yake na kwa watanzania wote walioguswa kwa namna moja au nyingine... *INNAH LILLAHI WA INNAH LILLAHI RAJUN*

0 comments: